Sio Arsenal tu, Premier League itamkumbuka Wenger akiondoka


Sio Arsenal tu, Premier League itamkumbuka Wenger akiondoka

wenger-epl

Na Joel Chuku

Vijana wa modern Era Ambao hasa sisi kutoka mataifa ya mbali tunashabikia timu kutokana na mfanikio yake kwakua in the first place tunakua hatupo connected exactly na hizo timu hadi ikiwa inakua bingwa na tunaifahamu huku Afrika ndio tunaipenda .

Vijana wa sasa tunaamini zaidi kwenye magoli kuingia nyavuni kuliko kwa mchezo mzima wa soka na of course hata managers wengi wa sasa kwenye soka ndio walivyo.

Dunia ya sasa technology imekuja huku ikiondoa uhalisia mwingi wa vitu, tunakosa vitu kua pure kuanzia vyakula tunavyokula mpaka hata aina ya burudani tunazopata.

Siku hizi ni kawaida sana kukuta msanii anaimba ila hajui kutumia hata kifaa kimoja cha muziki ni kawaida kutokana na dunia tuliyopo. Kijana wa sasa unakuta ana miaka 28 yupo kwa baba ni kawaida kutokana na dunia tuliyonayo  tumeacha fundamentals ya kuishi proper life kitambo sana ndio maana siwezi kushangaa kinachotokea hata kwenye soka ..

Arsene Wenger miaka 20 yake aliokaa arsenal au miaka yake zaidi ya 30 ya kufundisha soka mafanikio yake hayaoneshi kabisa ubora wake ni hivyo, kwasababu jamaa ni wa kizazi cha zamani anaishi kwneye dunia ya sasa.

Huwezi kumuweka kwa makocha bora ukiongelea kwa vigezo vya makombe ila Premier League itamkumbuka huyu jamaa akiondoka sio Arsenal tu ametoka zake hukon Japan kwneye club ya Nagoya alikuja na beautiful game, akaifanya Arsenal iwe HOME OF BEAUTIFUL GAME pale England maana alikuta vitu vingi tofauti.

Hata mwaka 2007 alipotaka kuachana na Arsenal cha kushangaza hakutaka kuachana na timu kwakuwa club haina hela ila ni kwakuwa tu hakuelewana na bodi ya Arsenal na hiyo kwake ilikua umhimu zaid.

Kama angetaka personal Achievement nadhani angesepa kitambo tu ila kwake hiyo haikua muhimu ilimradi mpira uchezwe tu na ni very loyal kwa watu wake hua ana commitment ambayo hapendi kuzivunja kiswahili hata club ilipokuja kuwa na hela still yupo vilevile anataka mpira uchezwe tu hataki kutumia hela kupita uhalisia wa mambo kwamchezaji mmojammoja anataka hela itumike sawasawa na ubora wenyewe kwa hili still huyu mzee anaishi old ways na ndio identity yake.

Sikuwahi ku-doubt ubora wake hata siku moja, siku zote huwa namchukulia bora ila kiukweli hata mimi ni kijana wa kisasa asiee japo nina amini kwneye fundamentals ya football kama Wenger na kutokana na hilo ndio maana ninaelewa ni kocha bora kiasi gani.

Ukiangalia makocha wengi wa kisasa wanaheshimiwa kwa mafanikio yao ila hawaheshimiwi kwa personalities na maturity  zao kwneye game  ni makocha wachache mno ambao wataheshimiwa kwa mafanikio yao na personalities zao kwa mfano Sir Alex Ferguson japo Ferguson hakupitia matatizo  kama ya Wenger pale Arsenal ila ni kocha ambaye alikua anaelewa pia nini maana ya football labda na wale wa Liverpool akina Shanky na yule mwenzie hawa ndio walikua wanautashi wa kuelewa game na principles za football japo hawa wa liverpool ni wazamani so obvious watakua hivyo tu  ila hawa akina Guardiola, Zidane, Mourinho hawatakuja kupata hiyo honour.

Hata ukiangalia kwa sasa sidhani kama kuna kocha yeyote pale Premier League kwenye interview zake hua anaulizwa general questions nje ya maswali ya kuhusu team yake kama huyu Arsene Wenger na siku zote anajua kutoa majibu sahihi..

Arsenal ina bahati kidogo ya kuwa na managers wenye genius brain awali alikua Herbert Chapman aliishape mno club hiyo na nina amini Wenger ana weza asipate heshima kama ya Chapman. Huyu Chapman alitengeneza karibia vitu vingi sana kuanzia jezi, soka uwanjani na kutupa mafanikio pia  na pia hata Highbury alitoa ideas zake ionekane vipi hata na chama cha soka cha FA kilikua kinamsikiliza mno huyo jamaa kwa ushauri jinsi ya kuifanya ligi zao ziwe bora mpaka zile za madaraja ya chini.

Chapman alikufa akiwa kocha wa Arsenal kwa kipindi ambacho tulifanya vizuri sana England na tulikua tunajiandaa kuwa bora kwa soka la Ulaya kiujumla ni kama Arsene Wenger club ilianza kuzingua kipindi ameshafanya vizur sana England na akiwa kwenye harakati za kuteka soka la Ulaya.

Wachezaji wengi mno wamekimbia pale Arsenal kutokana na club kutokua na direction nzuri ila huwezi sikia hata mmoja wa wachezaji hao anamsema vibaya Wenger wachezaji wenye chuki na Wenger ni wachache mno na mara nyingi wanakua na personal problems ambao haihusiani na ubora halisi wa  soka lao.

Hata mimi pia siamini kwenye imani kuwa kutumia hela nyingi ndio kupata mafanikio makubwa, tumia kiasi cha pesa kutokana na ubora halisi wa huduma utakayo pata na ukishanunua pia unatakiwa ujue kufanya integration nzuri wachezaji hao wafiti kwenye timu sometimes tatizo huwa sio kwa wachezaji tatizo linakuwa kwa vipi wanatumika ma kwenye principles hii Wenger anaisimamia vizuri mno ndio maana club inampenda .

Wenger ana class ambayo makocha wengi wa sasa hawana na hawata kuja kua nayo, kitu ninachopingana nae mpaka sasa still nina amini angeweza kununua quality flan ya wachezaji pasipo kutumia hela ambao wangekuja kuwa wazuri kuliko kundi flan la wachezaji aliowahi kuwanunua au kuwaamini.

Anaweza maybe asishinde Champions League mpaka anastaafu ila am sure mpaka wakati ukifika atakua ameiacha Arsenal mahali pazuri mno, kuna mashabiki wengine football kwao ni just groly days tu hawa hawataweza kuja kumuelewa manager kama wenger  ila wale mashabiki wengine ambao football ni maisha yao na wanajaribu kuulewa mpira ulivyo fundamentals hasa za mpira hawa ndio wanagundua ubora halisi wa Wenger.

Binafsi nimekua kiumri nikizungukwa na watazamaji mpira na jamii ya watu wanaopenda mpira, kiujumla nimezungukwa na wanamichezo tangu utoto mwangu na naelewa exactly nini maana ya football ndio maana sad days na groly days still nimekua naelewa ni nini anaifanyia timu yake.



Comments