Mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Manchester United ulichagizwa na kazi ya ziada iliyofanywa na golikipa wa Manchester United mhispania David De Gea kuokoa mchomo wa fundi wa kibrazil Phil Coutinho.
Dakika ya pili ya mchezo huo, De Geal aliiokoa timu yake kwa kuokoa mpira uliopigwa na Emre Can lakini kazi liyoifanya kuzuia kazi nzuri iliyofanywa na Coutinho ndiyo ilikuwa save ya maana katika mchezo huo.
Coutinho alijitahidi kupiga mpira kwa ustadi kwa kutumia mguu wake wa kulia nje kidogo ya box na mashabiki wengi waliamini mpira huo ulikuwa unatinga kambani.
Lakini ubora wa De Gea uliiweka United salama ikiwa ni miongoni mwa changamoto nyingi ambazo amefanikiwa kufaulu kwenye maisha yake ya soka akiwa Manchester United.
Tukio hilo lilionekana kuwa ndio lililowavutia mashabiki wengi walioshuhudia mchezo huo kuliko matukio mengine yoyote.
Comments
Post a Comment