GWIJI wa zamani              wa Manchester, Ryan Giggs amekiri kuwa anbamuonea huruma              nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney ambaye anahaha              kupata namba kikosi cha kwanza kwa klabu na timu ya taifa.
        Mchezaji huyo,              30, alianzishwa benchi na meneja wa muda wa Uingereza Gareth              Southgate Jumanne usiku katika sare ya 0-0 dhidi ya              Slovenia.
        Rooney pia              amekuwa miongoni mwa wachezaji wa akiba katika kikosi cha              Manchester United mechi tatu chini ya Jose Mourinho.
        "Namwonea              huruma," Giggs aliiambia ITV. "Kuelekea mwishoni mwa msimu              uliopita na kwa Uingereza majira ya joto alichezeshwa kama              kiungo kisha akaambiwa atacheza kama namba 9 au 10. Kwa              kiasi fulani alichanganyikiwa."
        "Namna pekee ya              kumrejesha kwenye kiwango ni mazoezi. Simuoni akicheza              kwenye namba moja, anakipaji cha kucheza kwenye nafasi              tofauti na uzoefu mkubwa."
        Rooney anatumaini              kurejea kwenye ikosi cha Manchester United Jumatatu usiku              dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield.
        
Comments
Post a Comment