Pogba ampa somo Mourinho ili aoneshe ubora wake



Pogba ampa somo Mourinho ili aoneshe ubora wake

1Paul Pogba amekiri kwamba angependa kuchezeshwa mbele zaidi kwenye klabu yake ya Manchester United na kusema kuwa sehemu anayocheza kwa sasa inamgharimu sana.

Mfaransa huyo alirejea Old Trafford kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya dunia mwezi Agosti mwaka huu, lakini mpaka sasa hajafanya yale hasa yaliyotarajiwa na wengi.

Wakati kocha wake Jose Mourinho akimchezesha namba tofauti na ile aliyoizoea, Pogba (23) anaamini kwamba kocha wake atambadilishia majukumu kwenye timu hiyo.

"Najaribu kuendana na hali halisi," alisema Pogba na kuongeza: "Mimi ni mchezaji ambaye napenda zaidi kucheza eneo la mbele."

"Kocha alinipa maelekezo, najaribu kuyafanyia kazi, napaswa kuachia mipira na kufanya jukumu la ukabaji zaidi."

"Kwa namna fulani inanigharimu kucheza tofauti, kama vile Andrea Pirlo. Natapaswa kucheza na kuwa makini muda wote kuhakikisha mipira yote inarudi na kuchezesha timu."



Comments