PEP GUARDIOLA APONDA STAILI YA MIPIRA MIREFU YA MANCHESTER UNITED



PEP GUARDIOLA APONDA STAILI YA MIPIRA MIREFU YA MANCHESTER UNITED
PEP Guardiola ameponda staili ya Manchester United ya kutumia mipira mirefu wakati akifafanua anachotaka kukiona kwa timu yake ya Manchester City.

City walilala 1-0 Old Trafford katika mechi ya EFL katikati ya wiki na ikaelezwa kwa Guardiola kwamba timu yake ilishindwa kucheza kwa staili yao kutokana na ukabaji wa kutumia kasi kubwa wa United.

 Guardiola hakulichukulia poa jambo hilo akisisitiza kwamba timu yake inaweza kucheza soka mbele kwa mbele lakini kikosi cha Jose Mourinho kimeshindwa kutokana na kupiga mipira mirefu juu, staili ambayo yeye kamwe hataitumia.

"Dhamira ya United ilikuwa ni mpira mrefu. Ukipoteza mpira unapogombea kwa hewani wanakufunga goli," alisema.


"Wakati mwingine unafungwa goli kwa sababu unalazimika kuanza kujenga mashambulizi kama haya. Na wakati mwingine unapiga mipira mirefu na unafungwa pia."


Comments