NEYMAR SASA HANUNULIKI, ASAINI MKATABA MPYA WA MIAKA MITANO BARCELONA ...thamani ya kuvunja mkataba wake ni pauni mil 225
NEYMAR amesaini mkataba            mpya wa miaka mitano kuendelea kuitumikia Barcelona na sasa            thamani ya kuununua mkataba wake ni pauni milioni 255.  
        Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alikutana na            rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu na kusaini            mkataba huo utakaofikia kikomo mwaka 2021.
        Kipengele cha kuununua            mkataba wake kimeongezeka kutoka pauni 171 hadi pauni milioni            200 ndani ya mwaka wa kwanza, lakini kitapanda hadi pauni            milioni 225 katika miaka mitatu ya mwisho.
        Neymar akishikana mkono na rais wa              Barcelona  Josep Maria Bartomeu baada ya kusaini mkataba              mpya
        Neymar              akishangilia bao lake dhidi ya Manchester City
        
Comments
Post a Comment