MUHOGO MCHUNGU ACHARUKA KUHUSU KUZUSHIWA KIFO



MUHOGO MCHUNGU ACHARUKA KUHUSU KUZUSHIWA KIFO
MWIGIZAJI mkongwe wa filamu, Abdallah Mkumbila "Muhogo Mchungu" anamsaka kwa udi na uvumba mtu aliyemzushia kifo kwenye mitandao ya kijamii ilihali yeye ni mzima wa afya tele.

Alisema kuwa, mitandao ya kijamii ni kama kisu, ukiitumia vibaya inaweza kusababisha madhara makubwa katika jamii na kuwataka watu waitumie vizuri ili wasilete madhara kwa jamii.

"Sijui huyo aliyezusha hayo mambo alikuwa na maana gani, kwani amezua taharuki kwenye familia yangu na katika jamii. 

Nataka kwenda TCRA ili niweze kumjua nani amefanya hivyo ili tumfikishe kwenye vyombo vya sheria," mwigizaji huyo alikiambia kipindi cha "Super Mix" cha East Africa Radio.


"Mimi ni mzima wa afya njema kabisa sio marehemu kama watu wanavyosema, nipo Bagamoyo na katika wiki mbili hizi sijasumbuliwa hata na mafua, nimesikia hizo tarifa za kifo changu na nimetumiwa mpaka picha."


Comments