KIUNGO wa Manchester City, Ilkay Gundogan ameiita Manchester United timu isiyo na adabu kwa kitendo ilichomfanyia Mjerumani mwenzake, Bastian Schweinsteiger.
Schweinsteiger alijiunga na Man United akitokea Bayern Munich majira ya joto mwaka 2015 na amecheza mechi 31 katika msimu wake wa kwanza katika soka la Uingereza.
Mkongwe huyo, 32, amekosa nafasi katika kikosi cha Jose Mourinho, hata hivyo Gundogan amebwatuka kuwa mashetani wekundu hawajamtendea haki mshindi huyo wa Kombe la Dunia.
"Naamini kwamba Manchester United inaweza kufaidika kwa asilimia 100 kutoka kwa Bastian Schweinsteiger," Gundogan aliiambia Sport Bild.
"Kama kila tunachosikia na kusema ni kweli, naweza kusema wamemvunjia heshima, yeye si mchezai yule wa awali, si Yule wa miaka 18 au 19."
Klabu kadhaa zimetajwa kuitamani huduma ya kiungo huyo mwenye uzoefu mkubwa, ikiwa ni pamoja na MLS ya Galax ambayo ilionyesha nia ya kumsajili mwishoni mwa mwezi uliopita.
Comments
Post a Comment