JUMAMOSI faulo mbaya kutoka kwa Enzo Perez dhidi ya Andres Iniesta iliwarusha roho mashabiki wa shoka ambao walihofia makubwa, lakini bahati kiungo huyo atakuwa nje kwa kati ya wiki sita ama nane tu, muda ambao ataiwahi Clasico.
Desemba 3, tarehe iliyopangwa kwa mechi ya kwanza kati ya Barcelona na Real Madrid msimu huu, iko wiki sita baadae.
Baada ya kurejea Barcelona akitokea Valencia ambako alifanyiwa vipimo zaidi, kiungo huyo, 32, anaweza kuanza program maalum ya matibabu.
Kiujumla Iniesta atakosa mechi saba za Barcelona, nne katika La Liga (Granada, Sevilla, Malaga, Real Sociedad) na mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya (Manchester City na Celtic) na mechi ya awali ya hatua ya 16 Bora ya Kombe la Mfalme dhidi ya Hercules.
Hata hivyo, kama Iniesta atahitaji wiki nane kupona, atakosa mechi tano zaidi na hatacheza hadi baada ya mapumziko ya kipindi cha Krismasi.
Mara ya mwisho Barcelona kuivaa Real bila ya "mchawi" wao huyo ilikuwani mwaka 2011 dhidi ya Jose Mourinho kwenyev Ligi ya Mabingwa Ulaya ambako Barca walishinda 2-0 kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.
Comments
Post a Comment