KABLA ya Ahamisi usiku, Paul Pobga alikuwa sawa na gari la kifahari lilofungiwa ndani. Lakini katika mchezo wa Europa League dhidi ya Fenerbahce, Mourinho akafungua geti na kulitoa hadharani 'gari' na kuliendasha huku akiwakoga majirani wenye wivu.
Mchazaji huyo ghali duniani kwa mara ya kwanza akaonyesha kile kilichofanya Manchester United imsajili kwa pauni milioni 89.
Pobga aling'ara vilivyo katika mchezo huo wa Europa League na kuiwezesha Manchester United kuibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya miamba hiyo ya Uturuki.
Licha ya Pobga kuzunguka uwanja mzima na kusambaza mipira kwa ustadi wa hali ya juu, lakini pia alifunga magoli mawili, moja likija kwa mkwaju wa penalti na liingine akiunganisha kwa umahiri pasi ya Lingard.
Kiungo alipiga pasi za uhakia 78 ukilinganisha na 38 alizotoa katika mchezo dhidi ya Liverpool Jumatatu usiku.
Paul Pogba aling'wakati ara jana Manchester United ikiiadhibu Fenerbahce
Paul Pogba alitupia magoli mawili
Pogba akifunga bao la kwanza kwa penalti
Comments
Post a Comment