KOCHA wa Bayern              Munich, Carlo Ancelotti amedai kuwa ameachiwa kazi nyepesi              na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola ambaye              amejiunga na klabu ya Manchester City.
        Ancelotti amesema              kuwa anaamini atafanikiwa katika klabu hiyo ya Bayern Munich              kutokana na Guardiola kuiwekea njia ya mafanikio klabu hiyo.
        Guardiola akiwa              katika klabu hiyo ya Bayern alifanikiwa kutwaa mataji saba              katika misimu mitatu ambayo aliitumikia ikiwa pamoja na              kutwa taji la Bundesliga.
        Ancelotti amedai              kuwa anavutiwa na uezo wa wachezaji hao ambao umeachwa na              kocha Guardiola.
        "Ni kazi nyepesi              sana kwa sasa katika klabu hii kwa kuwa nimewakuta wachezaji              wakiwa katika ubora wa hali ya juu."
        "Ninaamini ubora              wa timu hii umeachwa na Guardiola, nimeikuta timu ikiwa              katika ubora wa hali ya juu hivyo sina kazi kubwa ya              kuifundisha."
        "Misingi ambayo              imeachwa na Guardiola ninaamini siwezi kuiacha au              kuibadilisha kwa sasa kwa kuwa mizuri na itanipa mafanikio,              japokuwa nina mipango yangu ambayo ninaweza kuiweka hapa,"              alisema Ancelotti.
        Bayern Munich kwa              sasa inashika nafasi ya kwanza katika msimu wa Ligi ikiwa na              pointi 16 huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Hertha Berlin              ambayo ina pointi 13 baada ya timu hizo kucheza michezo              sita.
        "Ninajua kwamba              timu yangu inafanya vizuri. Nimekuwa nikiiangalia timu hii              kwa misimu mitatu iliyopita, hivyo kikubwa ni kuendelea na              kasi hii kwa ajili ya kuipa mataji," aliongeza.
        Kocha huyo mwenye              umri wa miaka 57 aliwahi kuzifundisha klabu kubwa duniani              kama vile AC Milan, Paris Saint-Germain, Real Madrid pamoja              na Chelsea.
        
Comments
Post a Comment