KIUNGO wa klabu              ya Rangers ya Scotland, Joey Barton anakabiriwa na adhabu              kwa kucheza kamari kinyume na sheria za soka nchini humo.
        Barton              anatuhumiwa na chama cha soka nchini Scotland kwa kuweka dau              mara 44 kati ya Julai 1 na Septemba 15, mwaka huu.
        Barton atarejea              katika klabu hiyo baada ya kufungiwa kwa wiki tatu kutokana              na utovu wa nidhamu.
        Chama cha soka              nchini humo, SFA kupitia sheria yake kifungu cha 33,              inakataza wachezaji, makocha, maofisa wa klabu na waamuzi              nchini humo kuweka dau kuhusu matokeo ya michezo popote pale              duniani. 
        Mwezi Mei, kiungo              wa Partick Thistle, Steven Lawless alifungiwa michezo sita              baada ya kuthibitika kuwa alicheza kamari ya michezo 513.
        
Comments
Post a Comment