JURGEN KLOPP ASEMA NI MAPEMA MNO KUITABIRIA LIVERPOOL UBINGWA



JURGEN KLOPP ASEMA NI MAPEMA MNO KUITABIRIA LIVERPOOL UBINGWA
HAKUNA ubishi Liverpool wazuri msimu huu acha kabisa. Wameanza vizuri msimu na wanaendelea kupeta wanavyotaka.

Hata hivyo pamoja na ubora wao wote huo, bosi Jurgen Klopp amesema ubingwa msimu huu kwa timu yake bado kabisa.

Ni sawa na kauli ya kukatisha tama, lakini kwa kocha huyo raia wa Ujerumani anaona Ligi ndio kwanza mbichi na kuongelea ubingwa wa kikosi chake ni sawa na kupoteza muda wakati huu.

"Reds" ni moja ya timu tatu za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, inakusanya pointi 20 ikiwa nyuma ya Manchester City na Arsenal kwa tofauti ya mabao.

Liverpool tayari imeshacheza na vigogo kama Arsenal, Tottenham Hotspur, Leicester, Chelsea na Manchester United katika mechi nane za kwanza msimu huu, lakini Klopp anasema ni mapema sana kufikiria ubingwa kwa sasa.

"Sijali. Ni masuala ya kawaida kwenye soka timu inapofanya vizuri watu wanaanza kuzungumzia nafasi ya ubingwa."

"Sishawishiki kuamini kila kinachozungumzwa na watu kuhusu sisi. Safari bado ni ndefu na kwa sababu hiyo huwezi kuzungumzia masuala ya ubingwa kwa sasa," alisema kocha huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari.


Comments