DEMU AMPONZA MCHEZAJI NEW ZEALAND… apigwa marufuku kucheza mchezo mmoja baada ya kuingia nae msalani
MCHEZAJI wa timu ya Raga ya New Zealand, Aaron Smith amepigwa marufuku kucheza mchezo mmoja baada ya kuingia msalani na mwanamke katika uwanja wa ndege mjini Christchurch.
Hiyo ni kinyume na kanuni za timu hiyo ya taifa.
Atakosa mchezo wa ubingwa wa Raga dhidi ya Afrika Kusini mjini Durban.
Kocha wa All Bracks, Steve Hansen amesema Smith mwenyewe amesikitishwa sana na kitendo hicho.
Hansen ameongeza kwamba mchezaji huyo wa miaka 27 anahisi kwamba ameivunja moyo timu yake, familia yake na mpenzi wake.
"Ameomba kwenda nyumbani kushughulikia masuala ya kibinafsi ambayo yameibuka kutokana na kisa hicho na tuna furaha kumsaidia katika hilo," amesema Hansen.
Kocha huyo amesema adhabu hiyo iliafikiwa na kundi la viongozi wa timu ambalo lilijumuisha wachezaji.
Smith amechezea New Zealand mashindano 54 tangu aanze kuwachezea mwaka 2012. Baadae mwaka 2012 alizuiwa kucheza kwa muda kwa kuvunja amri ya kutotoka nje.
Mwaka 2014 alituma picha yake ya utupu kwenye snapchat ambayo ilisambaa sana mitandaoni.
Comments
Post a Comment