BEKI wa kushoto wa timu ya taifa ya Uingereza, Danny Rose amesema Alan Shearer alikuwa sahihi kusema kuwa timu hiyo ya taifa itapatapa baada ya kujiuzulu kwa meneja Sam Allardyce.
Anasema kuwa sio jambo zuri kwa meneja kuondoka muda mfupi akiwa bado hajatimiza mikakati aliyojiwekea na hilo linaathiri pia wachezaji.
Rose alikuwa katika kikosi cha Uingereza kilichofunga Slovakia katika mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia chini ya uongozi wa Sam Allardyce.
"Nilimtumia ujumbe nikimshukuru kwa kunijumuisha katika kikosi chake na kunifanya kuwa na heshima nyingine katika ulingo wa soka la kimataifa. Nikamwambia pole sana kwa kupoteza nafasi yake na kumtakia kila la kheri mbeleni," alisema Rose.
Allardyce ameingia katika historia ya kukaa kwa muda mfupi katika timu hiyo kwa sku 67 tu, aliingia baada ya Roy Hodgson kubwaga manyanga alipotolewa mapema katika michuano ya Euro 2016.
Comments
Post a Comment