STRAIKA wa timu              ya Bayer Leverikusen, Javier Hernandez maarufu kwa jina la              "Chicharito" amesemekana kuwindwa tena na klabu za Ligi Kuu              ya Hispania La Liga.
        Shirika la habari              nchini humo AS liliripoti kuwa timu za Valencia na Sevilla              kwa sasa zinapigana vikumbo zikimwania nyota huyo raia wa              Mexico ili kuhakikisha zinapata huduma yake wakati wa              usajili wa majira ya baridi yajayo ya Januari, mwakani.
        
Comments
Post a Comment