AZAM FC HALI MBAYA YALAZIMISHWA SARE NA MTIBWA SUGAR


AZAM FC HALI MBAYA YALAZIMISHWA SARE NA MTIBWA SUGAR

yanga-vs-mtibwa-znz-3-640x360-1

Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar

Na.Alex Mathias,Dar es salaam.

Baada ya kutoka sare na Yanga,gonjwa la sare laendelea kuitafuna klabu ya Azam Fc ikicheza kwenye uwanja wa Azam Complex,Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam imetoshana nguvu sawa na Mtibwa Sugar kwa kufungana bao 1-1.

Dakika ya 2 Mshambuliaji mwenye mwili uliojengeka Rashid Mandawa aliwanyanyua mashabiki wa Mtibwa Sugar kwa kufunga bao safi kwa njia ya kichwa akiunganisha krosi ya Issa Rashind hata hivyo Azam walisawazishwa kupitia kwa kiungo wao mkabaji Himid Mau kwa njia ya penati baada ya beki wa Mtibwa kuunawa ndani ya 18.

Kwa matokeo hayo Azam wamefikisha pointi 13 wakati wapinzani wao Mtibwa wamefikisha jumla ya alama 16 nafasi ya nne hivyo baada ya mpira kumalizika wachezaji wa Azam wameonekana kuumizwa na matokeo hayo.

Kesho wekundu wa Msimbazi Simba watakuwa dimbani kucheza na Mbao Fc uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuendeleza rekodi ya ushindi ili wajiweke katika nafasi nzuri ya kufukuzia ubingwa ambao wameukosa miaka kama minne.

HAYA HAPA MATOKEO MENGINE YA JANA OKTOBA 19:

.Toto 0-2 Yanga

.Lyon 0-2 Majimaji

.Prisons 2-1 Stand

.Ruvu 1-1 Mwadui FC

.Ndanda 1-1 Mbeya City

.Azam 1-1 Mtibwa  (P.T)



Comments