JUMAMOSI hii litapigwa pambano la kukata na shoka la ligi kuu ya England jijini London kati ya matajiri wa jiji la Chelsea watakaokuwa wageni wa Arsenal kwenye dimba la Emirates.
Umemsikia kocha wa Arsenal, Arsene Wenger? Amesema siku hiyo hatokubali kuachia pointi tatu ziende kwa matajiri hao wakati anaijua timu hiyo kwa sasa ni ya kuungaunga.
Wenger amesema Chelsea bila nahodha wao John Terry ni kichochoro cha kuvunia pointi kwa kila timu, hivyo atahakikisha vijana wake wanabakiza pointi zote tatu.
"Najua Chelsea watataka kushinda Jumamosi, lakini naamini tutawashinda kwa sababu wanapomkosa Terry wanacheza ovyo kwenye ulinzi na tutalitumia pengo hilo kikamilifu," alitamba Wenger.
Chelsea wataingia dimbani wakikumbukia maumivu waliyoyapata Ijumaa iliyopita walipopigwa mabao 2-1 na Liverpool kwenye dimba lao la Stanford Bridge kikiwa ni kipigo cha kwanza kwa msimu huu katika Ligi Kuu.
Comments
Post a Comment