VIDEO- KOSCIELNY APIGA BONGE LA GOLI ARSENAL IKIPATA USHINDI KWA MBINDE DHIDI YA SOUTHAMPTON



VIDEO- KOSCIELNY APIGA BONGE LA GOLI ARSENAL IKIPATA USHINDI KWA MBINDE DHIDI YA SOUTHAMPTON

3Bao la dakika ya 90 la mkwaju wa penati kupitia kwa Santi Cazorla limeinusuru Arsenal kupata sare katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates dhidi ya Southampton baada ya kushinda mabao 2-1.

Southampton walianza kupata goli katika dakika ya 18 baada ya kipa wa Arsenal Petr Cech kujifunga mwenyewe kufuatia mpira uliotokana na adhabu ndogo uliopigwa na Dusan Tadic kugonga mwamba na kumgonga mgongoni.

Laurent Koscielny aliisawazishia Arsenal bao safi dakika ya 29 baada ya kupiga overhead kick nzuri baada ya mpira uliotokana na kona kuzagaazagaa langoni mwa Southampton.

Santi Cazorla ndiye shujaa wa Arsenal ambaye alifunga bao la pili kwa penati baada ya Olivier Giroud aliyeingia kutoka benchi kuchezewa madhambi na beki wa Southampton Jose Fonte.

Video ya magoli



Comments