VIDEO- JOSE MOURINHO AMEWATUPIA LAWAMA WACHEZAJI WAKE KWA KIPIGO CHA JANA


VIDEO- JOSE MOURINHO AMEWATUPIA LAWAMA WACHEZAJI WAKE KWA KIPIGO CHA JANA

1Jose Mourinho amewalaumu wachezaji wake wa Manchester United kuwa ndiyo sababu ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya mahasimu wao Manchester City kwa mabao 2-1.

Man United walijikuta wakipotezwa kabisa na vijana hao wa Pep Guardiola kwenye dimba lao la Old Trafford, na kujikuta wakiruhusu magoli mawili yaliyofungwa na Kevin De Bruyne na Kelechi Iheanacho.

Baada ya mchezo huo Mourinho alisema: "Wakati mwingine wachezaji huwavunja moyo mameneja wao."

Aliiambia Sky Sports: "Kipindi cha kwanza walikuwa vizuri zaidi yetu. Tulianza mchezo vibaya sana.

"Tulianza mchezo huku baadhi ya wachezaji wakicheza chini ya kiwango chao cha kawaida kuanzia kwenye suala la umakini mpaka kasi ya mchezo.

"Unahitaji kuwa na maamuzi ya haraka namna unavyocheza na unavyofikiri.

"Mchezaji mmoja au wawili hivi walikuwa hawapo kwenye kiwango kizuri na hali hiyo imeigharimu timu.

"Kiukweli, Nina wachezaji wawili au watatu hivi ambao kipindi cha kwanza, kama mchezo ungekuwa unachezwa sasa hivi na najua kinachoenda kutokea, nisingewachezesha, lakini hili ni soka na wakati mwingine wachezaji wanafedhehesha mameneja wao na wakati mwingine wanatupa sifa kubwa."

Hata hivyo Mourinho aliongeza: "Kwa hiyo lawama zote nibebeshwe mimi, mimi ndiye meneja na kosa ni langu kwasababu mimi ndiye niliyechagua kikosi."

Mourinho aliwaanzisha Jesse Lingard na Henrikh Mkhitaryan kwenye kikosi cha kwanza lakini aliwatoa wote baada ya kipindi cha kwanza kuisha baada ya kuonesha kiwango kisichoridhisha.



Comments