"Tatizo la pesa ndiyo linatusumbua na kupelekea kupoteza mechi zote nne, timu inakosa morali kwasababu hakuna pesa", kocha wa Majimaji FC Peter Mhina amesema baada ya timu yake kuchezea kichapo kwa mara nyingine kutoka kwa Yanga.
Majimaji imepoteza mechi zake nne za mwanzo wa ligi, Majimaji ilipoteza mchezo wake wa kwanza kwa goli 1-0 dhidi ya Prisons, ikafungwa 3-0 na Azam FC, kabla ya kupoteza tena 2-1 dhidi Mtibwa Sugar.
Tayari Majimaji imeruhusu magoli 9 katika michezo minne iliyocheza huku yenyewe ikiwa imefunga goli moja pekee.
"Ni mapema sana kusema timu itashuka daraja, bado kuna mechi nyingi tutajipanga na kuona namna gani tutapata ushindi katika michezo yetu ijayo ili tukae katika nafasi nzuri", alisema
Comments
Post a Comment