MOURINHO 'KUMSAJILI' DANNY DRINKWATER WA LEICESTER KWA PAUNI MIL 30 DIRISHA DOGO LA JANUARI



MOURINHO 'KUMSAJILI' DANNY DRINKWATER WA LEICESTER KWA PAUNI MIL 30 DIRISHA DOGO LA JANUARI

DANNY DRINKWATER ni chaguo jipya la Jose Mourinho katika usajili wa kushtua wa mwezi Januari utakaoigharimu Manchester United pauni milioni 30. 
Bosi huyo wa Manchester United ameshatumia pauni milioni 150 dirisha la kiangazi kuwasajili Paul Pogba, Eric Bailly na Henrikh Mkhitarayan, huku Zlatan Ibrahimovic akiwasili kama mchezaji huru.
Lakini Mourinho bado ameambiwa fungu lipo na sasa anamwania kiungo huyo Leicester City na England mwenye umri wa miaka 26.
Kiungo huyo alikuwa mchezaji wa Manchester United kuanzia mwaka 2008 kabla ya klabu hiyo haijamtema mwaka 2012.



Comments