MANCHESTER UNITED BADO KICHWA CHA PANZI …yapigwa 3-1 na Watford


MANCHESTER UNITED BADO KICHWA CHA PANZI …yapigwa 3-1 na Watford

LICHA ya kuanza Premier League kwa kishindo na kushinda mechi tatu mfululizo chini ya kocha Jose Mourinho, Manchester United imeanza kurejea kwenye enzi za kuchukua kichapo.

Timu hiyo imelambwa 3-1 na Watford katika mchezo mgumu wa Premier League uliochezwa kwenye dimba la Vicarage Road.  

Huo unakuwa mchezo wa pili mfululizo kwa United kupoteza katika Premier League baada ya kunyukwa 2-1 na Manchester City wikiendi iliyopita.

Lakini unakuwa mchezo wa tatu mfululizo kupoteza katika mashindano yote kufuatia kipigo cha 1-0 kutoka kwa Feyenoord  kwenye Europe League Alhamisi usiku.

Watford walikuwa wa kwanza kuandika bao kunako dakika ya 34 kupitia kwa Etienne Capoue kufuatia makosa ya mshambuliaji Anthony Martial aliyerejea nyuma kuokoa.

Mshambuliaji kinda wa Manchester United Marcus Rashford akasawazisha dakika ya 62 na kuamsha ari ya kusaka bao la ushindi.

Wakati United wakipeleka mashambulizi mfululizo kwenye lango la Watford, wakajikuta wanaruhusu bao la pili dakika ya 84 kupitia kwa Juan Camilo Zuniga huo ukiwa ni mpira wake wa kwanza kuugusa baada ya kutokea benchi.

Dakika ya 90 Watford wakapata penalti iliyopigwa na Troy Deeney na kuzaa bao la tatu.

Watford (4-4-2): Gomes 7; Cathcart 7, Britos 7.5, Prodl 8, Holebas 6.5; Janmaat 7 (Amrabat, 49, 7), Behrami 7, Capoue 7.5 (Zuniga 82), Pereyra 7; Deeney 7.5, Igahlo 6 (Success 90)

Manchester United (4-2-3-1): De Gea 6; Valencia 5.5 (Mata 62, 6), Smalling 5, Bailly 5.5, Shaw 6 (Memphis 85); Fellaini 5, Pogba 5; Rashford 7, Rooney 5, Martial 5 (Young 38, 6); Ibrahimovic 6
Etienne Capoue celebrates after scoring Watford's                opening goal in the first-half at Vicarage Road
Etienne Capoue baada ya kuipatia Watford bao la kwanza

Rashford was in a                      hurry to get the match underway once again after                      scoring United's second-half equaliser
Rashford akishangilia baada ya kuisawazishia United
Juan Zuniga celebrates after                  scoring Watford's late second goal with his first touch                  after coming on as a substitute
Juan Camilo Zuniga  akishangilia bao lake



Comments