Samatta akicheza kwa dakika 90 wakati klabu yake ya Genk ikicheza ugenini dhidi ya Standard Liege, ameishuhudia klabu yake ikishindwa kuchomoza na ushindi baada ya kuchapwa goli 2-0 game iliyochezwa Stade Maurice Dufrasne.
Dakika ya 11 Genk waliruhusu goli la kwanza lililofungwa na Belfodil na kudumu kwa dakika zote za kipindi cha kwanza.
Licha ya kocha wa Genk Peter Maes kufanya mabadiliko kwa kuwatoa wachezaji watatu Bryan Heynen na kumuingiza Susic huku Thomas Buffel akimpisha Trossard lakini bado mabadiliko hayo hayakubadili matokeo badala yake mambo yakazidi kuwa magumu.
Dakika ya 90 Genk wakaruhusu goli jingine safari hii Orlando Sa akikwamisha mpira kambani.
Genk inashika nafasi ya saba ikiwa na pointi 10 baada ya kucheza mechi sita ikishinda michezo mitatu, sare mbili na kupoteza mechi mbili.
Comments
Post a Comment