Liverpool wamefanya kile kinachoitwa kufuru dhidi ya Mabingwa Watetezi wa Ligi ya England Leicester City baada ya kushinda mabao 4-1.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na Roberto Firmino dakika za 13 na 89, Sadio Mane dakika ya 31 na Adam Lallana dakika ya 56.
Bao pekee la kufutia machozi la Leicester limefungwa na Jamie Vardy dakika ya 38.
Video ya magoli
Comments
Post a Comment