Kwa wale wote wenye mashaka na uwezo wa Cesc Fabregas wamepata majibu mazuri baada ya nyota huyo wa Hispania kufunga mabao mawili matamu ya 'extra time' yaliyoipa Chelsea ushindi wa 4-2 dhidi ya Leicester katika EFL Cup.
Mchezo huo ulilazimika kwenda hadi dakika 30 za nyongeza baada ya miamba hiyo miwili ya Premier League kutoka sare ya 2-2 katika muda wa kawaida.
Nyota wa kimataifa wa Japan Shinji Okazaki aliiduwaza Chelsea baada ya kuifungia Leicester mabao mawili ya kuongoza katika dakika ya 17 na 34.
Chelsea wakasawazisha kupitia kwa mabeki wake Gary Cahil dakika ya 45 na Cesar Azpilicueta dakika ya 50 kabla ya Cesc Fabregas kufanya vitu vyake dakika ya 92 na 94.
Leicester walilazimika kucheza pungufu kuanzia dakika ya 89 baada Marcin Wasilewski kulambwa kadi nyekundu.
Leicester 4-4-2: Zieler 6; Simpson 5, Wasilewski 4.5, Morgan 6, Chilwell 6.5; Schlupp 6, King 7, Drinkwater 7, Gray 6 (Amartey 90); Okazaki 7.5 (Ulloa 75, 6), Musa 6 (Vardy 76, 5).
Chelsea 4-2-3-1: Begovic 6; Azpilicueta 6, Cahill 5, Luiz 6, Alonso 5; Fabregas 8, Matic 6; Moses 5, Loftus-Cheek 5 (Costa 67, 6.5), Pedro 6 (Hazard 89, 7); Batshuayi 5.5 (Chalobah 80)
Cesc Fabregas amefunga mara mbili katika extra-time na kuisongesha mbele Chelsea katika EFL Cup
Cesc Fabregas akishangilia bao lake
Shinji Okazaki aliifungia Leicester City mabao mawili ya mapema
Comments
Post a Comment