Chelsea leo wameponea chupuchupu kupoteza mchezo wao dhidi Swansea baada ya kusawazisha goli dakika za majeruhi, katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliopigwa kunako Uwanja wa Liberty Stadium.
Chelsea walianza kupata goli kupitia kwa Diego Costa dakika 18 tu ya mchezo baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Oscar Emboaba.
Swansea wakasawazisha dakika ya 59 kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Gylfi Sigurdsson.
Swansea wakaongeza goli la pili dakika ya 62kupitia kwa Leroy Fer kabla ya Chelsea kusawazisha kupitia kwa Diego Costa mnamo dakika ya 81.
Dondoo Muhimu
- Ni wachezaji watano tu wamefanikiwa kufikisha mabao 35 kwenye Ligi ya England katika michezo michache kuliko Costa (58) – Andy Cole (41), Alan Shearer (42), Fernando Torres (52), Kevin Phillips (52) na Ruud van Nistelrooy (55).
- Goli la ufunguzi la Costa lilikuwa ni la 100 kwenye msimu wa 2016-17.
- Kulikuwa na gap la dakika mbili na sekunde 10 kwa magoli ya Swansea.
- Sigurdsson sasa amekuwa mchezaji wa Swansea kufunga magoli mengi zaidi kwenye Ligi ya England kuliko mchezaji yeyote kwenye klabu hiyo (26).
- Wachezaji 11 kati ya 13 waliocheza mchezao wa leo kwa Chelsea walipiga walau shuti moja-moja.
Comments
Post a Comment