YATHIBITIKA OSCAR DOS SANTOS BADO ANA MAISHA MAREFU CHELSEA


YATHIBITIKA OSCAR DOS SANTOS BADO ANA MAISHA MAREFU CHELSEA
NYOTA wa Brazil, Oscar dos Santos Emboaba Junior, bado ana maisha marefu ya kuichezea klabu ya Chelsea baada ya kuonyesha uwezo wake wa kuisaidia The Blues kupata ushindi katika mchezo wao wa mwisho katika ziara nchini Marekani.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 alipachika mabao mawili na kuifanya Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Milan ikiwa ni mwanzo mzuri wa kocha mpya, Antonio Conte na anafarijika kuona timu yake inafanya vizuri katika mchezo dhidi ya Milan ambayo ni timu nzuri.

Hata hivyo, Chelea iliwapa nafasi mastaa Diego Costa aliyekuwa majeruhi, N'Golo Kante aliyeingia akitokea benchi na Eden Hazard alipata nafasi ya kucheza dakika chache tu.

Kinda wa Chelsea, Bertrand Traore alifanikisha klabu yake kuongoza lakini jitihada zake zilifelishwa na kiungo Muitaliano, Giacomo Bonaventura, baada ya kusawazisha bao lake kwa kupiga moja kwa moja mpira wa adhabu.

Chelsea walikuwa na hali ngumu baada ya washambuliaji wa AC ilan kufanya mashambulizi ya mara kwa mara na kumpa kazi ya ziada Azpilicueta licha ya umahiri wa mlinda mlango Thibaut Courtois kulinda vizuri lango lake.

Licha ya Mbrazil Willian kudhibitiwa na Donnarumma, aliongezewa nguvu na Fabregas kabla ya mlinda mlango wa Milan kuchukua maamuzi ya kutoka ili kuokoa mpira ule.


Lakini katika kipindi cha pili, mabadiliko ya Oscar yalifanya matumanini ya Conte kurudi baada ya kuongeza nguvu na kupachika mabao mawili yaliyosababisha ushindi huo mnono.


Comments