Arsene Wenger amedhamiria kuendelea kumtumia Theo Walcott kama mshambiliaji wa kati licha ya mchezaji huyo kudai sasa anataka kubakia kama winga.
Baada ya miaka mingi ya kumshawishi kocha wa Arsenal kwamba anaweza kucheza kama mshambuliaji, Walcott aligeuza mawazo wiki iliyopita kwa kusema anataka kutambulika kama winga wa kulia.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 alianza kama mshambuliaji wa kati katika mchezo wa ushindi wa bao 8-0 dhidi ya Vicking ya Norway siku ya Ijumaa na kufunga bao moja na kupika moja.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema ataendelea kumtumia Theo Walcott kama mshambuliaji
Tangu asajiliwe Arsenal mwaka 2006, Walcott amekuwa akiumia mara kwa mara
"Ninaamini Walcott ana vigezo vyote vya kuwa mshambuliaji mkubwa," alisema Wenger
"Amekuwa mzuri anapokimbia na mpira, ni mchezaji mwenye akili na mmaliziaji mzuri.
"Si mkabaji mzuri hivyo naamini kutumia mbio zake katika thelusi ya mwisho ya uwanja kutazaa matunda mazuri zaidi".
Comments
Post a Comment