HATIMAYE Paul Pobga amewasili England kwaajili ya kukamilisha usajili wake wa rekodi ya dunia wa kujiunga na Manchester United kutoka Juventus.
Kurejea Old Trafford kwa kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa, kumekuwa ni gumzo la dirisha hili la usajili kutokana na danadana nyingi zilizozunguka dili lake la pauni milioni 110.
Pobga anarejea United - klabu iliyomtoa kwenda Juve kwa kulipwa kifuta jasho cha pauni 80,000 tu mwaka 2012.
Anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano na mshahara wa pauni 290,000 kwa wiki pindi atakapofuzu vipimo vya afya.
Paul Pogba akiwasili England tayari kwa vipimo vya afya Manchester United
Pogba akitabasamu
Pogba na msafara wake akiingia Aon Training Complex, Carrington kwenye uwanja wa Mazoezi wa Manchester United kwaajili ya vipimo vya afya
Pogba aliwasili Manchester kwa ndege akitokea New York kupitia Nice, Ufaransa
Pogba akiwa ndani gari la Manchester United aina ya Chevrolet Camaro
Mama mzazi wa Pogba naye pia yuko Yeo Moriba Manchester akimsindikiza mwanae
Hii ndiyo ndege iliyombeba Pobga
Comments
Post a Comment