MSHAMBULIAJI Sergio Aguero juzi alikosa penati mbili, moja ikipanguliwa na kipa na nyingine ikienda nje, lakini akatuliza kichwa na kufunga mabao matatu "hat trick" kuiwezesha Manchester City kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 nyumbani kwa Steaua Bucharest nchini Romania.
Ushindi huo katika mchezo wa kwanza wa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya umewaweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwani wanahitaji sare yoyote watakaporudiana Agosti 24 nyumbani kwenye dimba la Etihad, mjini Manchester.
Mabao mengine ya City katika mchezo huo yalifungwa na David Silva na Nolito ambapo kwa mara nyingine kocha Pep Guardiola alimchomesha mahindi benchi kipa Joe Hart.
Katika mchezo mwingine wa mechi ya kufuzu, Borussia Monchengladbach ya Ujerumani iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Young Boys ya Uswisi.
Comments
Post a Comment