Mchezo wa ligi ya Ubelgiji (Belgium Pro League) kati ya Gent dhidi ya Genk umemalizika kwa Genk kuchapwa bao 1-0 na kupoteza pointi tatu muhimu.
Genk ambayo inachezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilikuwa ugenini katika mchezo huo na kujikuta ikishambuliwa kwa asilimia kubwa ya mchezo huo.
Bao pekee liliipa ushindi Gent lilifungwa dakika ya 90 na Jeremy Perbet ambaye alikuwa mfungaji bora katika msimu uliopita.
Samatta aliingia dakika ya 66 kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis lakini hakuweza kutupia kambani katika mchezo huo hadi dakika 90 zikimalizika.
Mchezo huo ni wa pili katika ligi yenye timu 16 huku Genk ikiwa nafasi ya nane kwa pointi zake tatu baada ya kupata ushindi kwenye mechi yake ya kwanza katika ligi.
Jumamosi ya August 13 Gek itakuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani kucheza dhidi ya Waasland-Beveren.
Comments
Post a Comment