REAL MADRID YAWASILISHA OFA MPYA NEWCASTLE KWA AJILI YA MOUSSA SISSOKO


REAL MADRID YAWASILISHA OFA MPYA NEWCASTLE KWA AJILI YA MOUSSA SISSOKO
KLABU ya Real Madrid ya Hispania imepiga hatua katika nia ya kumsajili kiungo Moussa Sissoko kwa Newcastle United, baada ya kuwasilisha ofa mpya ya pauni mil 35.

Newcastele wamesema hawatambania Sissoco kwani wameshamsajili mrithi wake Mohamed Diam'e raia wa Senegal, lakini wanachokitaka ni fungu la kutosha.

Mbali ya kiasi hicho cha fedha ili kuilainisha Newcastle, Real imeahidi kuwatoa wachezaji wawili chipukizi, Mariano Diaz na Marcos Llorent, ili kuzipiku timu zinazomfukuzia ikiwa ni pamoja na Juventus, PSG, Everton, West Bromwich na Crystal Palace.


Comments