PHIL NEVILLE ASEMA POGBA ANASTAHILI KUNUNULIWA KWA PAUNI MIL 100 MAN UNITED



PHIL NEVILLE ASEMA POGBA ANASTAHILI KUNUNULIWA KWA PAUNI MIL 100 MAN UNITED
BEKI wa zamani wa Manchester United, Phil Neville anaamini kuwa staa anayewindwa na klabu yake hiyo, Paul Pogba anastahili kununuliwa kwa kitita cha pauni mil 100.

Man United wako mbioni kuvunja rekodi ya usajili kwa kutoa kitita hicho kumnunua Pogba mwenye umri wa miaka 23 na Neville anamini kuwa hawajapotea katika hilo.
"Nadhani watakuwa wamepata mmoja kati ya viungo bora duniani," alisema mkongwe huyo.


Pogba ambaye alitokea katika Academy ya Man United, alitimka Old Trafford mwaka 2012 na kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu Italia, Juventus na sasa mabosi wake hao wa zamani wanataka kumrejesha kwa dau litakalovunja rekodi.


Comments