MCHEZAJI kinda wa Galatasaray ya Uturuki, Bruma, amepagawa baada ya kuelezwa na Mourinho kuwa nahitajika Old Trafford.
Bruma mwenye miaka 21, ambaye anaweza kucheza kama mshambuliaji au winga, alisema alipokea taarifa yenye kuvutia wikiendi iliyopita bada ya Mourinho kumwambia anamwitaji.
Mchezaji huyo alitoka uwanjani baada ya mchezo wa kirafiki baada ya Galatasaray na Gothenburg kwenye dimba la Ullevi Stadium, ambapo wawakilishi wa Mourinho walimwita na kumkutanisha nae.
"Mourinho alinishika mkono baada ya kumfikia akanitingisha kwa kunipongeza akasema nimeonyesha kiwango kizuri na kwamba siku hiyo alikuja kuthibitisha juu ya uwezo wangu na kwamba amenikubali," alisema Bruma.
Aliweka wazi kuwa Mourinho amemwambia atamsajilki lakini atamwacha aendelee kukipiga Galatasaray ili kujiongezea uzoefu na kujiamini, kabla ya kuanza kuitumikia United msimu ujao.
Comments
Post a Comment