MOURINHO AWATAKA WENGER, KLOPP WAACHE KUMWANDAMA



MOURINHO AWATAKA WENGER, KLOPP WAACHE KUMWANDAMA
KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa wanavyomkosoa makocha Arsene Wenger na Jorgen Klopp si sahihi kwa sababu ana maamuzi yake binafsi kama kocha.

Kocha wa Arsenal, Wenger na kocha wa Liverpool, Klopp wamekuwa wakihoji juu ya matumizi ya pauni mil 100 yaliyofanywa na United kwa Pogba.

"Ni mambo ambayo nikifanya si sahihi lakini wakifanya wengine inaonekana kawaida," alilalamika Mourinho.
Kocha huyo wa United aliongeza kuwa atamsainisha kiungo bora ndani ya siku chache – Bila shaka ni kiungo wa Juventus, Pogba (23).
"Tuna wachezaji 22 sasa," alisema. "Tutakuwa 23."
"Ni mchezaji wa Juve mpaka aondoke rasmi. Dirisha la usajili linafungwa Agosti 31. Tunajaribu kila tuwezavyo kumaliza shughuli yetu kwenye soko kabla ya kufikia Agosti 14."

Kocha wa Arsenal, Wenger alisema kuwa thamani hiyo kwa Pogba ni ya kiwendawazimu, wakati kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alisema hawezi kutumia fedha nyingi kama hizo kwa mchezaji mmoja hata kama alikuwa ana fedha ambazo ni nyingi kupita kiasi.

Lakini Mourinho alisema kuwa hakufurahishwa na jinsi wenzake walivyomkosoa, huku akijitetea na jinsi ambavyo amekuwa akimfanyia kiungo Bastian Schweinsteiger.
Nahodha wa zamani wa Ujerumani Schweinsteiger, 32, amekuwa akifanya mazoezi peke yake, suala lililopelekea mmoja wa wanachama wa umoja wa wachezaji Ulaya kusema kuwa Mourinho anastahili kufungwa jela kwa ajili ya uonevu.


"Niliamua kufanya maamuzi yangu, Niacheni. Hilo linatokea kwenye kila klabu duniani," alisema kocha huyo wa zamani wa Chelsea.


Comments