JOSE MOURINHO amemkosesha amani Juan Mata baada ya kumpiga benchi dakika 27 tu tangu alipomwingiza uwanjani katika mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Leicester City.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania aliuzwa na Mourinho kutoka Chelsea kwenda United mwaka 2014 hiyo ikiwa ni baada ya kusugulishwa benchi sana licha ya kocha huyo kumkuta Mata akishikilia tuzo ya mchezaji bora wa klabu.
Kitendo cha Mourinho kumwingiza Mata dakika ya 63 na kumtoa dakika ya 90 akimpisha Henrikh Mkhitaryan, kimezua maswali mengi juu ya hatma ya nyota huyo aliyenunuliwa na David Moyes kwa pauni miliono 37.1.
Mata alionekana wazi kukerwa na hatua hiyo na ilibidi wasaidizi wengine wa benchi la ufundi watumie sekunde kadhaa kumfariji.
Hata hivyo, Mourinho amejaribu kufafanua kwa kusema kuwa alimwingiza Mkhitaryan katika sekunde za lala salama ili kuongeza udhibiti wa mipira ya juu iliyokuwa ikipigwa na Leicester.
Mourinho anasema Mata alielewa na kukubali maamuzi hayo ingawa mwanzoni alionekana kuchanganyikiwa.
"Nilifanya jambo ambalo si jema kulifanya ambalo - kumtoa Mata katika dakika ya mwisho - Lakini sasa amenielewa na ameridhika.
"Nisingeweza kumtoa Fellaini au Ibra. Fellaini na Ibra walikuwa muhimu sana uwanjani kwa kuzuia mipira ya kurusha ya Rory Delap na tulitaka kushinda mchezo.
"Sheria ya mchezo ule ilituruhusu kufanya mabadiliko mara sita, nilikuwa nimeshafanya mabadiko mara tano na nilitaka kuuchelewesha mchezo.
"Nililazimika kumtoa mchezaji mwenye umbo dogo zaidi kwa sababu tulitarajia mipira ya juu zaidi. Mata alikuwa mwenye umbo dogo zaidi.
"Lakini alicheza vizuri sana. Alifanya kile nilichohitaji. Tunataka kushinda na mwisho wa siku kila mtu alikuwa na furaha."
Mata akionekana kuchanganyikiwa baada ya kutolewa nje
Juan Mata akifarijiwa baada ya kutolewa
Mata akiendelea kufarijiwa
De Gea akimfariji Mata baada ya mchezo
Mwisho wa siku kila mtu alifurahi ...Mata akifurahia Ngao ya Hisani
Comments
Post a Comment