Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa United kushinda 2-1, Ibrahimovic akaruka juu na kuunganisha kwa kichwa krosi ya Antonio Valencia hadi wavuni kukiwa kumesalia saba za mchezo.
United walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 32 kupitia kwa mshambuliaji wake chipukizi Jesse Lingard aliyefunga bao bora la mechi kutokana na juhudi zake binafsi za kuuchambua msitu wa mabeki wa Leicester kwa chenga tamu kabla ya kumtungua kipa Schmeichel.
Leicester City wakafunga bao lao kunako dakika ya 52 kupitia kwa mshambuliaji wake hatari Jamie Vardy kufuatia makosa ya kiungo Marouane Fellaini.
Manchester United (4-2-3-1): De Gea 6.5, Valencia 6.5, Bailly 7, Blind 7, Shaw 7 (Rojo 69), Carrick 6.5 (Herrera 61), Fellaini 6, Lingard 7.5 (Mata 63, Mkhitaryan 90+3), Ibrahimovic 6.5, Rooney 6 (Schneiderlin 88), Martial 6 (Rashford 70)
Leicester City (4-4-2): Schmeichel 6.5, Simpson 6.5 (Hernandez 63), Huth 6 (Ulloa 89), Morgan 5, Fuchs 6.5 (Schlupp 80), Mahrez 6, Drinkwater 7, King 6.5 (Mendy 63), Albrighton 6 (Gray 46), Okazaki 6 (Musa 46), Vardy 7
Wachezaji wa Manchester United na Ngao ya Hisani
Zlatan Ibrahimovic akishangilia goli lake
Ibrahimovic akishangilia na Mata na Rooney
Jesse Lingard (wa pili kushoto) akipiga mpira unaompita kipa wa Leicester na kuwa goli la kwanza kwa United
Lingard (katikati) na mbwembwe na kufurahia goli
Jamie Vardy anasawazisha
Makosa ya ukabaji ya Marouane Fellaini (kushoto) yakatoa mwanya kwa Vardy kuisawazishia Leicester
Comments
Post a Comment