MANCHESTER UNITED YAKATAA KURUDIA MAKOSA YA POBGA, YAMTOA JANUZAJ KWA MKOPO ...mwenyewe aliomba auzwe, ambebesha lawama Mourinho



MANCHESTER UNITED YAKATAA KURUDIA MAKOSA YA POBGA, YAMTOA JANUZAJ KWA MKOPO ...mwenyewe aliomba auzwe, ambebesha lawama Mourinho
on track. 
The                21-year-old flourished in Manchester when he was brought                through by David Moyes

Adnan Januzaj anajiandaa kutua Sunderland kwa mkopo ingawa mwenyewe alitaka kuuzwa jumla na Manchester United kufutia kukosa kwake namba katika kikosi cha kwanza.

Januzaj amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha marizevu tangu alipoambiwa uso kwa uso na kocha Jose Mourinho kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha wachezaji 26. 

Hata hivyo inaaminika kuwa nyota huyo wa Ubelgiji alikataa kushirikiana chumba cha kubadilishia nguo na wachezaji hao wa chini ya miaka 21 (U-21) kwa madai kuwa wakati anafika Carrington (Kambi ya United) tayari alishavaa kwaajili ya mazoezi na mara moja amewahi kubalishia nguo choooni.

Januzaj amekereka kwa namna ambavyo Mourinho hakumpa nafasi ya kuthibitisha ubora wake hasa baada ya kumkodisha mwalimu wa mazoezi ya kuongeza nguvu wakati alipokuwa mapumzikoni kiangazi hiki.

Aidha, kinda huyo mwenye umri wa miaka 21, hakuwa na furaha kwa namna ambavyo hakushirikishwa kwenye maamuzi ya jezi yake namba 11 aliyoirithi kwa Giggs kuhamishiwa kwa Anthony Martial.

Manchester United inahofia kumuuza Januzaj na kurudia makosa waliyoyafanya kwa Pobga ambaye walimtoa bure na kulazimika kumnunua kwa rekodi ya dunia baada ya kwenda kung'ara Juventus. 

Januzaj anakwenda kuungana na kocha wa zamani wa United David Moyes huko Stadium of Light, pamoja na wachezaji wenzake Paddy McNair na Donald Love ambao nao waliuzwa Sunderland.

Moyes alimpa Januzaj mechi ya kwanza United mwaka 2013 kabla hajasaini mkataba mpya wa miaka mitano. 
Adnan Januzaj is set to leave              Old Trafford to join Sunderland on loan after feeling              humiliated
Adnan Januzaj anajiandaa kutua Sunderland kwa mkopo
Januzaj told Jose Mourinho                  he wanted a permanent exit but will not be granted his                  wish
Januzaj alimwambia Jose Mourinho anataka kuondoka jumla Manchester United lakini ombi lake hilo limetupwa


Comments