KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Luis Nani amempa sifa kiungo Paul Pogba kwa kuwa kwenye hatua za mwisho za kurejea Old Traffod na kusema kuwa matarajio yake ni kuwa atafanya vyema mara yake hii ya pili akiwa chini ya kocha Jose Mourinho.
Alisema: "Pogba ni mchezaji mkubwa, hakuna shaka juu ya uwezo wake. Anaweza kufanya vizuri."
"Fedha kwa sasa sio mpango wowote, sijui kiasi gani klabu imelipa kumnunua mchezaji. Sitaki kuzungumzia fedha zake za usajili isipokuwa ni mchezaji wa maana."
"Timu yoyote itakayomnunua itaeza kupata huduma bora kutoka kwake."
Kiungo huyo ambaye anatarajiwa kufanya vipimo vya afya leo jijini Manchester, jana Jumamosi picha zilimuonyesha akiondoka kwenye ukumbi mmoja wa sherehe kwenye jiji la New York huku akiwa na rapa wa Marekani, Drake.
Rapa huyo Mmarekani na mchezaji huyo ghali zaidi duninai, wameonekana kukutana mara kadhaa wiki hii na kula bata pamoja, huku Pogba akimkabidhi Drake jezi ya Juventus yenye inalake nyuma.
Na hii ni baada ya kuhudhuria tamasha kwenye viwanja vya Madison Square.
Pogba amekuwa gumzo kipindi hiki chote cha usajili wakati sasa akikaribia kukamilisha dili lake la pauni mil 100 kwa kurejea tena Old Trafford, lakini hilo halijamzuia kula bata baada ya kuitumikia klabu na nchi yake kwenye michuano ya Euro 2016.
Comments
Post a Comment