'KWA ALICHOMFANYIA BASTIAN SCHWEINSTEIGER ...JOSE MOURINHO ANASTAHILI KUFUNGWA JELA'



'KWA ALICHOMFANYIA BASTIAN SCHWEINSTEIGER ...JOSE MOURINHO ANASTAHILI KUFUNGWA JELA'

JOSE MOURINHO angepaswa kuswekwa jela kwa kumfanyia unyama Bastian Schweinsteiger, hiyo ni kwa mujibu wa mmoja wa wanachama wa umoja wa wanasoka unajulikana kama FifPro.
Kocha huyo mpya wa Manchester United hamuoni Schweinsteiger kama sehemu ya mipango yake na akaamua kumpeleka kiungo huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 32 kwenye kikosi cha 'marizevu'.
Dejan Stefanovic mwanachama wa FifPro kutoka Slovenia, akaiambia BBC kuwa hatua ya Mourinho haikuwa ya kiungwana na alisatahili kuchukuliwa hatua za kisheria.
"Mourinho anatengeneza mfano mbaya. Ningekuwa mimi ningemburuza mahakamani," anaeleza Stefanovic.
Dejan Stefanovic ambaye ni mwanasheria anaeleza zaidi: "Ni unyanyasaji. Kwa Slovenia ingetosha kumshtaki Mourinho na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.
"Schweinsteiger anapaswa kwenda kwenye chama cha wanasoka wa kulipwa na kufungua mashtaka na mimi pia ntaomba Mourinho aadhibiwe.

"Wachezaji  wa kikosi cha kwanza wanastahili kufanya mazoezi chini ya makocha wa kikosi cha kwanza katika eneo moja na kwa wakati mmoja kwa wachezaji wote.

"Na hilo ni jambo linalopaswa kufanywa katika kila klabu na inastahili kuandikwa katika sheria na FIFA".




Comments