KOCHA CLAUDIO RANIERI ASEMA HAKUNA NAFASI YA LEICESTER KUPOROMOKA LIGI KUU ENGLAND



KOCHA CLAUDIO RANIERI ASEMA HAKUNA NAFASI YA LEICESTER KUPOROMOKA LIGI KUU ENGLAND
KOCHA Claudio Ranieri amesema hakuna nafasi ya Leicester kuporomoka katika mbio zake za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England, kama ilivyokuwa kwa Chelsea msimu uliopita.

The Blues ilitwaa ubingwa mwaka 2015 lakini ilikuwa na mwanzo mbaya mwaka uliopita, hatua iliyosababisha kutimuliwa kwa kocha Jose Mourinho, kabla ya timu hiyo kumaliza nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi.

Kwa namna ambavyo Lesester ilifanikiwa kutwaa ubingwa ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kupigana kufa na kupona kujinasua kushuka daraja, mabingwa hao ambao leo wanavaana na kikosi kipya cha Mourinho, Manchester United kwenye Ngao ya Jamii kwenye uwanja wa Wembley, wanaamini msingi waliojijengea utawasaidia kutetea ubingwa wao.

Ranieri anataka makubwa zaidi msimu huu. "Wakati ninapojenga kitu fulani kamwe hakibomoki," alisema kocha huyo mzoefu raia wa Italia.


"Falsafa yangu ni kutazama nyumba yangu si ya wengine. Ni muhimu kwa kile kinachotokea hapa. Nyumba yangu ni safi sana na ipo wazi. Taratibu tumejaribu kujenga ghorofa ya kwanza na ya pili. Msingi ni imara sana."


Comments