KOCHA BENITEZ AMUONYA MOUSSA SISSOKO ASITHUBUTU KWENDA REAL MADRID



KOCHA BENITEZ AMUONYA MOUSSA SISSOKO ASITHUBUTU KWENDA REAL MADRID
BOSI wa Newcastle United, Rafael Benitez amemuonya straika Moussa Sissouko kuacha mpango wa kutaka kutua Real Madrid.

Sababu ya onyo hilo ni kile alichodai kocha huyo kuhofia kwenda kuua kiwango chake kwani ushindani wa namba ndani ya Madrid ni mkubwa.

Sissoko amekuwa katika rada za Real Madrid tangu kumalizika kwa michuano ya Euro 2016 iliyofanyika nchini Ufaransa.

Katika michuano hiyo, Sissoko alionyesha kiwango cha hali ya juu hivyo kuzivutia timu mbalimbali ikiwemo Madrid.

Sissoko mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akiwindwa na mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa dau la euro mil 40.

"Natambua Real wanataka kuja kwangu. Ninawasubiri, najua wanakuhitaji sana kwa sasa."

"Lakini ninachoweza kuona ni kwamba ndani ya Madridi kuna ushindani mkubwa wa namba."

"Unaweza ukafurahia kwenda kule leo, lakini kesho ukaenda kujutia uamuzi wako, lakini itakuwa tayari umeshachelewa," alisisitiza Benitez.
Hata hivyo, Benitez alithibitisha kuwa klabu yake ya Newcastle haitakubali kumuuza straika huyo chini ya dau la euro mil 40, kwani bado ana mkataba wa miaka miwili kamili.

"Nimemwambia Moussa, tunafahamu mambo yanavyokwenda ndani ya soka la kisasa na hatua ya kukurupuka sio njia njema, bali ni kutafakari," amenukuliwa bosi huyo wa zamani wa Los Blancos.


Madrid wameingia katika mbio za kutaka kumnasa Sissoko kufuatia hatua yao ya kumkosa Pogba ambaye tayari ametua katika kikosi cha mashetani wekundu wa jiji la Manchester.


Comments