KUSUASUA kumuachia kiungo Paul Pogba kunakomfanywa na Juventus kumemkera kocha Jose Mourinho ambaye amesema "isiwe taabu".
Katika kile kinachoonekana kama kususa, Mourinho alisema: "Siwezi kumzungumzia Pobga kwa sasa kwa sababu bado ni mchezaji wa Juventus, lakini ni wazi kuwa tutasaji mchezaji mmoja hivi karibuni.
"Sipendi kuzungumzia wachezaji wa timu nyingine na sipendi makocha wengine wawazungumzie wachezaji wangu. Lakini tufanya usajili wa mchezaji mkubwa."
Mourinho amekereka kuona suala la uhamisho wa kumrudisha Pogba Old Trafford umechukua muda mrefu.
Hata hivyo Mourinho anategemea kuwa suala la Pobga litafikia tamati wikiendi hii.
Comments
Post a Comment