JOSE MOURINHO ASEMA ALICHOKIFANYA KWA SCHWEINSTEIGER SAHIHI ...adai panga ni lazima ili kupisha nyota wapya
Jose Mourinho            amejitetea juu ya uamuzi wake wa kumtosa kiungo mkongwe            Bastian Schweinsteiger na kusisitiza kuwa anataka kufanyabkazi            na wachezaji 23 Manchester United.
        Mourinho amekuwa            kikaangoni baada ya kumlazimisha Mjerumani huyo mshindi wa            Kombe la Dunia kufanya mazoezi na kikosi cha chini miaka 23            (U-23). 
        Kocha huyo mpya            wa United amejitetea kuwa alichokifanya ni sahihi na kwamba            anapaswa kupiga panga kikosi chake ili kupisha wachezaji wapya            wanne aliowasajili hadi muda huu.
        Jose                Mourinho amejitetea kwa kile alichomtendea Bastian                Schweinsteiger
        Kiungo                mkongwe wa Ujerumani alilazimishwa kufanya mazoezi na                kikosi cha pili wiki iliyopita
          "Ninapaswa kufanya            maamuzi yangu. Ni hivyo tu," alisema Mourinho alipoulizwa juu            ya alichokifanya kwa Schweinsteiger.
        "Kilichofanyika            ndicho kinachofanyika katika kila klabu ulimwenguni, ni kocha            ndiye anayeamua juu ya kikosi chake".
        
Comments
Post a Comment