GUARDIOLA AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUTULIA NA WAKE ZAO SIKU MOJA KABLA YA MECHI


GUARDIOLA AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUTULIA NA WAKE ZAO SIKU MOJA KABLA YA MECHI
KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amewataka wachezaji kuwepo majumbani mwao na familia zao siku moja kabla ya mechi, badala ya kukaa kwenye hotel au viwanja vya mazoezi.

Utaratibu huo unamfanya Guardiola kuifanya Man City kuwa klabu ya kwanza ya Ligi Kuu England kulala katika viwanja vya mazoezi tangu walipofungua City Football Academy mwishoni mwa mwaka 2014.

Awali Man City walikuwa wakikaa hotelini karibu na viwanja vya mazoezi kama mahasimu wao, Manchester United katika mechi wanazochezea nyumbani.


Guardiola alisema: "Kama hawatapumzika hawatakuwa makini siku ya mechi, hivyo watapoteza kazi zao kwa kucheza vibaya. Mimi sio polisi ninawahukumu wachezaji wangu kwa kazi wanayoifanya na sio maisha yao binafsi."


Comments