CRISTIANO RONALDO AKUBALI KUONGEZA MKATABA WA HADI 2021 REAL MADRID



CRISTIANO RONALDO AKUBALI KUONGEZA MKATABA WA HADI 2021 REAL MADRID
TAARIFA kutoka katika klabu ya Real Madrid zimedai kuwa staa wao, Cristiano Ronaldo amekubali kuongeza mkataba utakaomfanya kubaki klabuni hapo hadi mwaka 2020 au 2021.

Imeelezwa kuwa winga huyo wa kimataifa wa Ureno anajiandaa kukutana na wakala wake, George Mendes na rais wa Madrid Florentino Perez ili kukamilisha mchakato huo.

Mshindi huyo mara tatu wa Ballon d'Or alikuwa akitajwa kutimka Bernabeu, hasa baada ya kutokuwa kwenye ubora wake katikati ya msimu uliopita.


Kwa mujibu wa taarifa hizo, Ronaldo, Mendes na Perez watakutana Agosti 10 ikiwa ni baada ya nyota huyo kurejea kutoka mapumzikoni.


Comments