KOCHA mpya wa              Chelsea, Antonio Conte amemtengea pauni mil 55 winga wa              klabu ya Lazio ya Italia, Antonio Candreva.
                Mchezaji huyo              mwenye miaka 29 amemwambia mlinzi mwenzake wa timu ya taifa              ya Italia, Leonardo Bonucci kwamba anatamani kwenda kucheza              soka nchini Uingereza ambako kuna ushindani mkubwa tofauti              na Italia.
        

Comments
Post a Comment