ZLATAN IBRAHIMOVIC APEWA JEZI NAMBA 9 MANCHESTER UNITED …Paul Pogba abakiziwa namba 6, Anthony Martial mmmh!
Zlatan Ibrahimovic amekabidhiwa jezi namba 9 Manchester United huku aliyekuwa akiimiliki namba hiyo Anthony Martial akipewa jezi namba 11.
Mshambuliaji huyo wa Sweden amezitumikia jezi namba 8,9 na 1o katika maisha yake ya soka na ilitarajiwa kuwa angekumbana na namba tofauti na hizo tatu ndani ya Manchester United kutokana na ukweli kuwa tayari jezi hizo zilikuwa zinamilikiwa na wachezaji wengine.
Lakini sasa Martial anahamia jezi namba 11 wakati Adnan Januzaj aliyekuwa akiitumikia namba hiyo, anapewa jezi namba 15. Juan Mata anabakia na namba 8 yake na Wayne Rooney anaendelea kuimiliki jezi namba 10.
Ibrahimovic ametupia picha ya jezi No 9 kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika: "Nimechagua namba 9."
Wachezaji wengine wapya wa United Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan, wamechukua jezi namba 3 na 22.
Jezi namba No 6 imeachwa wazi -haina mwenyewe - pengine imeachwa kwaajili Paul Pogba ambaye huwa anaivaa jezi hiyo katika klabu yake ya Juventus.
Ibrahimovic ametupia picha ya jezi No 9 kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika: "Nimechagua namba 9."
Orodha mpya ya wachezaji wa Manchester United na namba zao za jezi
Comments
Post a Comment