- Get link
- X
- Other Apps
ZLATAN IBRAHIMOVIC ni sasa ni mchezaji wa Manchester United.
Mara baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 kukamilisha usajili wake Old Trafford, akasema yupo tayari kupenyeza kumbukumbu nzuri England kupitia Manchester United.
Ibrahimovic anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Jose Mourinho ambapo nyota huyo alikiri kufurahia kujiunga na Manchester United.
Mourinho aliyefanya kazi na Ibrahimovic katika Inter Miland, amesema usajili huo hauhitaji maelezo yoyote na kwamba uwezo na ubora wa takwimu za mshambuliaji huyo zinajileza zenyewe.
Zlatan Ibrahimovic sasa ni mchezaji wa Manchester United
Ibrahimovic amesaini mkataba wa mwaka mmoja Old Trafford
Mchezaji huyo alifuzu vipimo vya afya Ijumaa na kusaini mkataba wa mwaka mmoja utakaomwingizia pauni 250,000 kwa wiki.Ibrahimovic ametua Manchester United bure baada ya kumaliza mkataba wake Paris St-Germain."Nimefurahi kuwa hapa, nitahakikisha nafanya makubwa hapa na kutengeneza kumbu kumbu nzuri", alisema Ibrahimovic mara baada ya kusaini Manchester United.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment